Utangulizi wa kozi
Hii ni kozi ya masomo 15. Itakuonesha mambo muhimu ya Biblia, ujumbe wa Mungu kwako.
Kila somo linafuatwa na maswali. Utapata msimamizi ambaye ataangalia majibu yako na ambaye utaweza kumuuliza maswali ya ufuatiliaji. Msimamizi wako ataonesha mwitikio kwa maswali yako ndani ya masaa 24-48. Mwishoni wa kozi utapokea cheti kama tu ushiriki wako wa kozi utamridhisha msimamizi wako.
Tunakushauri uwe unasoma somo 1 au 2 kwa siku. Hii itakuruhusu kufikiri kwa kina kuhusu mambo ya kiroho yaliyomo katika somo, na kuendeleza ushirikiano na msimamizi wako kwa kuzungumzia maswali yako na maisha yako ya kiroho. Inafanya viziri zaidi kama unatumia majuma kadhaa kusoma kozi yote. Hata hivyo tunategemea utaandika kila kitu na kukikusanya wewe mwenyewe bila kutegemea vifaa vya akili mnembo/bandia (AI) kama chatGPT.
Tunatumaini unaifurahia kozi, na kwamba itakusaidia kusogea karibu na Mungu!
Mwanafumzi kuhusu kozi hii:
“Msaada mkubwa kwangu kwenye kozi hii ilikuwa ni pale msimamizi wangu aliponisaidia na alipojibu maswali yangu hivyo nilielewa jambo fulani zaidi. Na ninashukuru sana kwa hilo.”
Masomo
-
Uumbaji
-
Anguko
-
Nuhu na Garika
-
Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu
-
Kuhama toka Nchi ya Utumwa
-
Sheria
-
Sadaka
-
Daudi
-
Kuzaliwa kwa Yesu
-
Yesu, Mungu Kweli
-
Yesu, Mwokozi Ambaye Haendani na Matazamio Yetu
-
Kuteseka kwa Yesu
-
Kufa na Kufufuka kwa Yesu
-
Kupaa kwa Yesu na Kuja/Kumiminwa kwa Roho Mtakatifu
-
Hatua Zinazofuata