Karibu kwenye kozi ya Maisha ya Yesu! Tazama maisha ya Yesu kutoka katika injili ya Luka, kwenye filamu iliyo na wafuatiliaji/watazamaji wengi katika historia ya dunia. Kuna masomo 15, kila moja lina kipande cha filamu, ikifuatiwa na maswali. Utapata msimamizi ambaye atatazama majibu yako na ambaye unaweza kumuuliza maswali ya ufuatiliaji. Msimamizi wako mara zote atasahihisha masomo yako kwa kipindi cha masaa 24-48.
Tunakushauri ukusanye siyo zaidi ya somo moja au mawili kila muda unapojifunza. Hii atakuruhusu kufikiri kwa kina kuhusu mambo ya kiroho ndani ya masomo, na kuendeleza uhusiano na msimamizi wako kwa kuzungumza kuhusu maswali yako na maisha yako ya kiroho. Inafanya vizuri zaidi kama unatumia majuma kadhaa kufanya kozi nzima. Kwa hiyo tunategemea uandike kila kitu wewe mwenyewe na kukikusanya bila kutegemea msaada wa zana za akili mnembo (AI) kama vile ChatGPT.
Tunatumaini utafurahia kozi, na hiyo itakusaidia kusogea karibu kabisa na Mungu!